FILE LA KANTE: Wazazi wa Kante walihamia Ufaransa wakitokea Mali.
Mambo hayakuwa mazuri sana kwao. Alipoanza maisha ya shuleni alipenda sana kucheza mpira wa rugby
Kante ni mtoto wa kwanza na hivyo alitumia muda mwingi kupambana kusaidia na wazazi wake waliokuwa ombaomba.
Kijiji cha Kante wengi wso walikuwa wasafisha mitaro na usafi wa jiji. Kiujumla waliishi uswahilini.
Kante alikuwa anzunguka jiji la Paris kwa zaidi ya kilometa 20 kwa siku kutafuta makopo na kwenda kuyauza ili kupata kipato
Kazi hiyo haikusaidia familia yao zaidi waliandamwa sana ukali wa maisha kutokana na ufukara wa kipindukia
Wakati wa kombe la dunia mwaka 1998 Kante alikuwa na miaka 7
Hakubahatika kuona mchezo wowote wa kombe la dunia
Aliishia kusikia majina makubwa ambao wengi walikuwa wahamaiaji kutoka Afrika kama yeye.
Ilimpa faraja kuwa ipo siku anaweza kupitia njia hiyo. Waokota makope wenzake walimuona chizi kwa kuwa na ndoto zile
Abadani Kombe la dunia ilikuwa fursa kubwa kwake kimaisha kwani alikuwa mfagiaji nje ya viwanja
Makopo yalipatikana kwa wingi sana bishara lilipamba moto
Alihakikisha anatembelea viwanja vingi kupata makopo ya kutosha
Baada ya Kombe la dunia shule ilimshinda baada ya kukosa ada
Akiwa na miaka 8 akajiunga na klabu ndogo ya mtaani kwao ya JS Suresness.
Wakamwona kioja kwenye timu kwani alidumaa sana halafu kafupi sana.
Wachezaji walimcheka, wakidhani hakataweza kucheza dakika 90.
Mwanzoni alipewa dakika 10 za mwisho lakini akastaajabisha wengi
Mwalimu wake anasema alifika kila sehemu ya uwanja. Alikuwa anacheza kama kichaa.
Kuna wakati kocha alimwambia asicheze sana akihofia asije akapata matatizo uwanjani.
Hakushangilia walipotwaa kombe. Kutokana na umasikini wakamwajiri awe anafundisha watoto ili aweze kusaidia familia yake kwa kibarua hicho
Baada ya baba yake kufariki, akijitokeza msamaria mwema Pierre Ville ambaye alimua kuchukua majukumu ya Kante
Pierre akaanzisha safari ya Kante katika soka la kulipwa. Kilichofuata ni historia.
0 Comments