MWANAMKE NI HAZINA YA MAISHA NA MAENDELEO YA MWANAUME.

👉 mwanamke katika jamii  wanahusika kwa mambo mbalimbali ya maisha. Inaelezwa ya kwamba hakuna mafanikio ya mwanaume bila mwanamke,nami hilo naliweka bayana kuwa ni kweli na mara nyingi imekuwa hivyo.Zipo faida nyingi ambazo zinatokana na mwanamke kama vile; kulea familia kwa ukaribu zaidi,kuweka muunganiko mzuri kwenye familia na jamii,kuleta chachu ya utafutaji kwa mme wake kwa kuzingatia hatua za maendeleo ya familia,kuleta furaha ndani ya ndoa na familia,kudumisha upendo kwenye ndoa,kuijenga heshima ya familia n.K.  Pia hakuna faida ambayo haina hasara kwa mfano :- mwanamke anaweza kuwa chanzo cha umaski kwa kushindwa kuhendo hali iliopo kwenye ndoa,anaweza akawa malaya na kujali pesa za mume wake kuzifanya kama ndizo za kufanyia starehe za kibinafsi.Hata hivyo jela la maisha mara nyingi hubebwa na mikono ya mwanamke.Jamii ya sasa iko kwenye mikono ya mwanamke na utandawaziuko mikoni mwa mwanamke na ndio maana mitandao ya kijamii imepata mwitikio mkubwa kupitia wao. Faida ni kutambua utu na mambo ya kidunia lakini hasara ni kuwa pale mwanamke hujikita katika mambo yasio faa na kusabisha mambo mengi kuwa hovyo.

Post a Comment

0 Comments